Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barker afichua kinachoikabili Yanga

BERKER Pict


KOCHA wa Simba, Steve Barker amesema kikosi hicho hakina presha yoyote katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara, akisisitiza kuwa kilichopo kwa sasa ni kuhakikisha timu inaendelea kushinda michezo yake iliyobaki.


Simba iliyopo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi na pointi 58 tofauti ya pointi mbili tu dhidi ya watani zao Yanga iliyopo kileleni na pointi 60 timu zote zikiwa zimecheza mechi 25 bado ina nafasi ya kutwaa ubingwa msimu huu endapo Yanga itashindwa kuibuka na ushindi kwenye michezo mitano iliyobaki.


Simba hijatwaa ubingwa kwa misimu minne mfululizo huku ukienda kwa watani wao Yanga na kwa msimu huu inaonekana kuwa kwenye nafasi nzuri ya kurudisha ufalme wake endapo itachanga karata zake vizuri. Akizungumza na Mwanaspoti, Barker raia wa Afrika Kusinia amesema mabadiliko hayo yametokana na maandalizi mazuri na usajili wa dirisha dogo ulioiongezea timu ubora na ushindani wa nafasi, kitu ambacho kimefanya wafanikiwe kushinda michezo kadhaa mfululizo.

“Tunataka kuwa klabu yenye utambulisho wake. Kila siku mazoezini tunafanya kazi kuhakikisha Simba inakuwa na namna yake ya kucheza bila kujali tunakutana na nani, jambo la kwanza hatutaki kujipa presha ya ubingwa, tunafahamu ili tuchukue kombe tunatakiwa kushinda michezo yetu, hilo ndiyo muhimu zaidi,” amesema Barker.

Kocha huyo alieleza kuwa wachezaji waliosajiliwa mwezi Januari akiwemo Clatous Chama, Nickson Kibabage na Libasse Gueye, Anicet Oura wameongeza nguvu ndani ya kikosi kutokana na namna walivyoendana haraka na mfumo wa timu.

“Wachezaji tuliowaleta walikuwa na manufaa makubwa. Wameongeza ushindani na kutupa chaguo nyingi zaidi katika maeneo mbalimbali ya uwanja tunaamini kwenye ubora wa kila mmoja na hawa ndiyo nguzo yetu,” amesema.

Barker amesema licha ya ushindani mkali wa kuwania ubingwa, ndani ya Simba hakuna hofu yoyote kwani kikosi hicho kimejikita katika kucheza mechi moja baada ya nyingine huku kikisaka ushindi kwenye michezo iliyosalia kwa mbinu kali zaidi ya ilivyokuwa mwanzoni mwa mzunguko wa pili.

“Hatuangalii sana yanayotokea kwa wengine. Tunachotaka ni kuendelea kucheza vizuri na kushinda mechi zetu. Nadhani presha ipo zaidi kwa timu nyingine kuliko Simba, sisi hatujali, mara nyingi ukiwa kileleni unakuwa na presha kuliko timu inayoshika nafasi ya pili au ya tatu,” amesema kocha huyo. Barker alijiunga na Simba Desemba 19,2025 akitokea Stellenbosch ya Afrika Kusini, kocha huyo anakuwa wa tatu kuifundisha Simba msimu huu baada ya Fadlu Davids na Dimitar Pantev, lakini kikosi chake kwa sasa kikiwa kimeshacheza michezo 25 kwenye msimu huu, kimeshinda mechi 17, wametoka sare saba na kupoteza moja wakiwa na pointi 58, wamefungwa mabao 10 na kufunga 45.