Barbara, Manara wanasa kwenye mtego wa Simba na Yanga

Friday May 20 2022
Barbara PIC
By Evagrey Vitalis

Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itakutana kesho Mei 21, 2022 jijini Dar es Salaam kusikiliza mashauri mawili yaliyowasilishwa mbele yake na klabu za Simba na Yanga.

Yanga ikimlalamikia Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez kwa madai kutoa shutuma zisizo za kweli kupitia Metro FM ya Afrika Kusini, Nayo Simba inamlalamikia ofisa wa Yanga, Haji Manara kwa madai ya kutoa shutuma zisizo za kweli dhidi ya klabu yao kupitia mtandao wake wa kijamii.

Barbara na Manara watafikishwa mbele ya Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) hapo kesho kutoa ushahidi wa shutuma anazodaiwa kuzitoa wakati akihojiwa na na Kituo hicho cha redio huko Afrika Kusini hivi karibuni.
Baada ya kusikiliza malalamiko hayo mwenyekiti wa kamati ya maadili alielekeza Sekretarieti ya TFF kuhakikisha walalamikiwa wote wamepewa mashtaka dhidi yao pamoja na mwito wa kuhudhuria mashauri hayo ambayo yataanza kusikilizwa Mei 14, 2022.

Hivyo, kikao cha kesho ni mwendelezo wa Kamati ya Maadili ya TFF kusikiliza mashauri hayo.

Advertisement