Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barbara aapa lazima kieleweke kwa Mkapa

Muktasari:

OFISA Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema; “Nina imani na maandalizi ambayo yamefanyika ndani ya timu tunachosubiri ni muda na kuona vijana wetu wanapambana kwa kiasi gani ili kuondoka na ushindi.”

OFISA Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema; “Nina imani na maandalizi ambayo yamefanyika ndani ya timu tunachosubiri ni muda na kuona vijana wetu wanapambana kwa kiasi gani ili kuondoka na ushindi.”

“Tumetoa bonasi kubwa kwa wachezaji wetu ila siwezi kusema ni kiasi gani, lengo letu kuu ni kutengeneza na kuwapa morali wachezaji ili waweze kutupatia ushindi mnono dhidi ya watani wetu Yanga,” alisema

Kocha wa Simba, Didier Gomes alisema kikosi chake kinawachezaji wengi bora ambao wanaweza kwenda kuamua matokeo ya mchezo huo tofauti na wale ambao wanapatikana katika timu pinzani.

Gomes alisema kuna mchezaji kama Feisal Salum ndio anaweza kuwa hatari zaidi lakini kwao kuna wengi zaidi kama wakiwa katika ubora watashinda.

Alisema kikosi chake kuna wachezaji bora kama Luis, Chama, Mugalu, Bocco, Wawa, Onyango, Manula, Kapombe, Tshabalala na Lwanga ambao wanaweza kuamua mchezo.

“Benchi la ufundi kwa ujumla tumejipanga vizuri, wachezaji wako kwenye morali kubwa na ni matumaini yangu kuwa tutaibuka na ushindi,” alisema Gomes na kuongezea;

“Nawaheshimu Yanga na kocha wake Nabi, nakutana naye kwa mara ya kwanza kwenye ligi lakini hilo halitatuzuia kufanya vizuri kwani tuko tayari kuwapa furaha mashabiki wetu.”

Kipa chaguo la kwanza nchini, Aishi Manula alisema mechi hizo si kama zina mambo mengi kama ambavyo wengi wanadhani bali ni maandalizi mazuri ndio yanawapa ushindi.

Manula alisema kama ambavyo wachezaji wa Simba wameonekana wengi wapo katika hali na morali nzuri ya kuipigania timu kuhakikisha inapata ushindi katika mchezo huo mkubwa.

“Ni wakati mzuri kwetu kama wachezaji kuonyesha ubora na thamani ya kikosi chetu, tumefanya mazoezi mazuri na morali ya kila mchezaji iko juu kueleka mchezo huo kiufupi ni kwamba tuko tayari kushinda,” alisema Manula na kuongezea;

“Kama ambavyo tumefanya vizuri katika mashindano ya kimataifa tumepanga kulionyesha jambo hilo katika mashindano haya ya ndani tena katika mechi kubwa dhidi ya Yanga.

“Ambacho naamini timu iliyo bora katika mechi hii ndio itakwenda kupata ushindi na si jambo lingine zaidi ya hilo,” alifafanua Manula ambaye tangu amejiunga na kikosi cha Simba hakuna mechi dhidi ya Yanga ambayo alikuwepo na akaikosa.