Banda aitanguliza Simba

DAKIKA 45 za kipindi cha kwanza zimemalizika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kwa Simba kupata uongoza bao 1-0 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.
Bao la Simba limefungwa na Peter Banda dakika ya tisa ya mchezo kufuatia pasi safi iliyopigwa na mshambuliaji Kibu Denis.
Simba waliendelea kulishambulia lango la Geita huku viungo Raymond Massota na Juma Mahadhi wakionekana kuwa watulivu mbele ya Jonas Mkude na Larry Bwalya ambao wameonekana kutawala kwa ukubwa eneo la katikati ya uwanja.
Dakika ya 20 Geita walifanya mashambulizi huku washambualiaji wake Daniel Lyanga na George Mpole wakikosa utulivu wa kumalizia nafasi.
Licha ya Simba kufanya mashambulizi mengi ila mabeki wa Geita Jonathan Mwaibindi na Oscar Masai wameonyesha utulivu kwenye idara hiyo.
Dakika ya 35, kipa wa Geita Khomeiny Abubakary aliokoa mpira uliokuwa unaelekea langoni mwake kufuatia shuti lililopigwa na John Bocco akipokea pasi iliyopigwa na Peter Banda.
Kinachoigharimu Geita katika kipindi hiki cha kwanza ni ngome imara ya Simba kwenye eneo la ulinzi wa kati ikiongozwa na Kennedy Juma na Joash Onyango.
Mpaka kipindi cha kwanza kinatamatika Simba wameonekana kutawala mchezo na kuwaacha Geita Gold wakiwa na maswali mengi ya kujibu katika kipindi cha pili.