Pablo abadili gia Simba ikiwavaa Geita

KOCHA mkuu wa Simba, Pablo Franco ameendelea kufanya mabadiliko kwenye kikosi chake kinachoikabili Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Winga Peter Banda na beki wa kushoto Gadiel Michael ni miongoni mwa wachezaji walioanza kwenye mchezo wa leo tofauti na kikosi kilichocheza Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows ya Zambia.
Kikosi kinachoanza ni Aishi Manula, Shomari Kapombe, Gadiel Michael, Joash Onyango, Kennedy Juma, Jonas Mkude, Peter Banda, Larry Bwalya, John Bocco, Kibu Denis na Ibrahim Ajibu.
Wachezaji wa akiba ni Beno Kakolanya, Erasto Nyoni, Mohamed Hussein 'Tshabalala', Pascal Wawa, Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga, Meddie Kagere, Bernard Morrison na Yusuph Mhilu.
Simba inashuka uwanjani ikiwa nafasi ya pili na alama 14, huku upande wa Geita Gold wakiwa nafasi ya 15, na pointi tano.