Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baiskeli tu imempa ulaji Richard Laizer

Muktasari:

Baada ya kushiriki mashindano mengi nje ya Tanzania hasa katika nchi ya Rwanda alikoshiriki mashindano ya Tour of Rwanda, aliwakuna wazungu ambao walitamani kumdhamini katika kazi zake na kumtafutia timu nje ya nchi.

SOKA, riadha na ngumi ndio michezo ambayo imepewa kipaumbele sana hapa nchini, lakini kuna michezo mingine yenye ulaji haijapewa kipaumbele ila ikiwekewa mikakati, basi itawasaidia wengi.

Richard Laizer ni mmoja kati ya waendesha baiskeli wenye majina makubwa Tanzania ambaye yupo kwenye timu ya taifa ya mchezo huo na amefanikiwa kupata fursa ya kuitumikia timu nje ya nchi.

Alianza mchezo huu mwaka 2005 akiwa na umri wa miaka 16 chini ya baba yake mdogo aitwaye Samwel Laizer ambaye alimshawishi amfundishe mchezo huo tena akipewa baiskeli aina ya Phonex ambayo ilimzidi nguvu.

Baada ya kushiriki mashindano mengi nje ya Tanzania hasa katika nchi ya Rwanda alikoshiriki nashindano ya Tour of Rwanda, aliwakuna wazungu ambao walitamani kumdhamini katika kazi zake na kumtafutia timu nje ya nchi.

“Mwaka 2012 nilifanikiwa kumpata meneja raia wa Italia aitwaye Nicholous Morganti ambaye alinifanyia mpango wa kujiunga na Timu ya MTN–Qhubeka ya Afrika Kusini ambayo ilinipa mkataba wa miaka miwili tangu 2012 hadi 2014.”

Akiwa kwa Madiba alifanya kazi ya ziada kwa kuwa hakwenda kutalii, bali kupiga kazi na alifanikiwa kwenda kushiriki mashin-dano katika nchi mbalimbali zikiwemo Brazil, Ujerumani, Italia, Uswis, Misri na Uingereza.

Baada ya kufanya kazi yake kwa weledi na kutamba vilivyo akiwa na timu ya MTN–Qhubeka, hatimaye mwishoni mwa mwaka 2015 alifanikiwa kutua Ujerumani kwenye timu ya Stradalli Bike Aid.

“Nilipomaliza mkataba na MTN sikuona haja ya kuendelea nayo licha ya kunishawishi kwa kutaka kuniongezea mshahara, lakini hatimaye nikaona lazima nibadili upepo kwa sababu nilipenda kwenda Ujerumani kwenye timu mpya ambaye malipo yake yalikuwa mazuri zaidi,” anasema.

Licha ya kupata mpunga mkubwa pia mazingira ya kazi yalichangia kwenda Ujeruman kuliko kubaki Afrika Kusini licha ya kwamba ndio walimfungulia milango na kutambulika nje ya Bara la Afrika.

Taizo kubwa lililonikumba Stradalli Bike Aid upatikanaji wa kibali cha kukaa moja kwa moja kama ilivyokuwa Afrika Kusini, hivyo likuwa akipewa cha miezi mitatu kila mara anapokaribia kwenda kwenye mashindano.

“Nchi za wenzetu tofauti sana na huku kwetu Afrika, kule kuna watu wengi ambao wanaingia kwa njia ambazo sio halali, hivyo hata unapopewa kibali unapewa kwa masharti.”

Mashindano ya Afrika ameshiriki zaidi ya mara tatu Mwaka 2011 yalifanyika Eritrea, mwaka 2012 Afrika Kusini na Mwaka 213 Misri, na mwaka 2011 pia alishiriki Mashindano ya Tour of Rwanda.

Mwaka 2014 alijitosa kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyka Scotland kabla ya kutimukia Brazil kwenye Mashindano ya Tour De Reo, pia ameshiriki Mashindano ya Moonstar ya Ujerumani na Ufaransa amewahi kushiriki Mashindano ya Paris Budgie. Laizer anasema amepata mafanikio makubwa sana kwenye mchezo wa kukimbia kwa baiskeli.

“Nawasihi wazazi wasiwakataze watoto wao kushiriki mchezo huo.

“Mchezo si soka peke yake, iko mingine ambayo inaweza kuwasaidia vijana kuweza kujijenga kimaisha,” alimalizia Laizer.