Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bahati abadilisha watatu Biashara United

Kocha wa Biashara United, Vivier Bahati amefanya mabadiliko ya wachezaji wanne katika kikosi chake kitakachoanza leo dhidi ya Yanga.

Biashara United itavaana na Yanga katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza saa 10 jioni.

Katika kikosi hicho nyota wanne walioanza katika mcheoz uliopita waliopoteza 2-1 dhidi ya Namungo wamepanguliwa na kuwekwa wengine.

Nyota hao ambao leo wameanzia benchi ni Collins Opare, Aniseth Revocatus na Boniphace Maganga ambaye alipata majeraha katika mchezo huo.

Wapya walioanza leo ni Ibrahim Ndunguri, Ambrose Awiyo na Salum Kipaga huku kipa namba moja, James Ssetuba na Deogratias Mafie wakiendelea kukosekana kutokana na majeraha.

Kikosi kitakachoanza leo dhidi ya Yanga ni Daniel Mgore, James Mwashinga, Christian Zigah, Ramadhan Chombo, Atupele Green, Abdulmajid Mangalo, Leny Kissu, Mpapi Nassibu, Ambrose Awiyo, Ibrahim Ndunguri na Salum Kipaga.

Kikosi cha akiba ni Edson Nyakwesi, Mathew Odongo, Collins Opare, Kassim Mdoe, Derick Mussa, Shaban Ada, Benson Masige, Taro Donald na Abdallah Madirisha.