Azam yarejesha jembe lao Mcameroon

Muktasari:
Kingue ambaye alikuwa akikichezea kikosi hiko msimu uliopita aliondoka baada ya uongozi wa Azam kutomuongezea mkataba.
KIUNGO Stephen Kingue amerejea nchini na kusaini mkataba wa miezi sita kukitumikia kikosi cha Azam FC.
Kingue ambaye alikuwa akikichezea kikosi hiko msimu uliopita aliondoka baada ya uongozi wa Azam kutomuongezea mkataba.
Baada ya Mwanaspoti kupata taarifa hizo lilimtafuta na alikiri kumalizana na uongozi huo wa wanalambalamba.
"Nipo Tanzania nimeamua kusaini tena hapa kwasababu muda ulikuwa unaenda na sikuwa na ofa nyingine zaidi ya Azam," alisema.
Usajili huo unazidi kuimalisha safu ya kiungo cha Azam inayoongozwa na Salum Aboubacary 'Sure Boy', Mudathir Yahya na Frank Domayo.