Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam yamtimua Lwandamina na benchi la ufundi

Azam yamtimua Lwandamina na benchi la ufundi

Muktasari:

  • Azam imeachana na kocha huyo baada ya sare 0-0 dhidi ya Kagera Sugar.

UONGOZI wa klabu ya Azam Fc umewatimua kazi benchi zima la klabu hiyo baada ya kutoka sare 0-0 dhidi ya Kagera Sugar mchezo uliochezwa jana katika uwanja wa Chamazi.
Benchi la Azam linaongozwa na kocha mkuu George Lwandamina na msaidizi wake Bahati Vivier.
Mwanaspoti baada ya kuzipata taarifa hizo lilimtafuta Lwandamina na alikiri kupokea taarifa hizo huku akiweka wazi yupo njiani kwenda kuonana na mabosi wake.
"Nimepokea taarifa hiyo lakini naenda kuonana na viongozi wa klabu, ni maisha yetu ya mpira," amesema Lwandamina.
Kocha huyo mwezi uliopita alitoka kuongezewa mwaka mmoja wa kuendelea kuiongoza timu hiyo lakini mabosi wake wameamua kuuvunja mkataba huo.
Azam mpaka sasa wanashika nafasi ya saba wakiwa na pointi 11 waishinda mechi tatu,  sare mbili na kupoteza mechi tatu.