Azam yaichapa Mbuni Arusha

Azam FC imeifunga Mbuni FC  mabao 2-0 katika mchezo wa kurafiki uliopigwa jijini Arusha.

Mechi hiyo imepigwa katika Uwanja wa Sheik Amri Abeid unatumika na timu hizo kama maandalizi ya mechi zao za zinazokuja za Ligi Kuu na Championship.

Azam ilitangulia kupata bao kupitia Prince Dube dakika ya 42 na bao la pili limefungwa na Lusajo Mwaikenda dakika ya 45 kabla ya kipenga cha mwamuzi Athumani Kado wa Arusha kusikika kuashiria tamati ya dakika 45 za mchezo.

Kipindi cha pili, kilianza kwa mabadiliko kufanyika ambayo hata hivyo hayakuzaa matunda.

Timu ya Azam wanautumia mchezo huo kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida Big Stars baada ya kuifunga timu ya Arta solar ya Djibouti 2-1 katika mchezo wa kirafiki.

Nao Wanajeshi wa Mbuni FC wanajiandaa na mchezo wao wa Champioship dhidi ya Stand United ya Shinyanga utakaopigwa Jumamosi Arusha baada ya kutoka suluhu ya 1-1 na Biashara United ya Mara katika mchezo uliopita.