Azam hawana jambo dogo

Azam hawana jambo dogo

Muda mfupi kuanzia sasa (saa 8:00 mchana), Uwanja wa Azam Compex unaweza kujaa kutokana na wingi wa mashabiki waliongia.

Hadi kufika saa 8:00 mchana muonekano wa Uwanja wa Chamazi ulikuwa umejaa tayari na sehemu iliyobaki ni ndogo tu.

Sehemu ambayo ilikuwa imebaki na hakuna mashabiki ni kusini mwa uwanja lilipo nyuma ya hili upande wenye luninga inayoonyesha matokeo.

Bado mashabiki wanaendelea kumiminika kwa wingi na pengine Uwanja unaweza kujaa muda wowote kuanzia sasa hadi mashabiki wengine kusimama.

Bado burudani za wasanii wala aina yoyote ile hainafanyika hapa Azam Complex ila shangwe na mashabiki limezidi kuwa kubwa na kuzidi kukiminika ndani ya uwanja.