Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam FC yalia na waamuzi

Kocha mkuu wa Azam FC, Bruno Ferry amewataka  waamuzi kuongeza umakini ili kutenda haki kwa timu zote.

Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo dhidi ya Coastal Union,  Bruno amesema ligi ya Tanzania imekuwa kubwa na inafuatiliwa sehemu kubwa nje ya nchi lakini inaangushwa na waamuzi.

"Baada ya mchezo pale Dodoma, sikuongea kwa sababu sikuwa na video lakini sasa naweza kuongea kidogo kwa sababu nimeiona video na ninayo hiyo video,"amesema Bruno

"Kuna kitu nataka kusema tunaelewa kwamba siyo kitu rahisi kuwa mwamuzi kwa sababu unatakiwa kuamua haraka na kwa sasa mchezo uko kasi sana.

"Hii ni kitu kigumu sana...ni kitu ambacho tunaelewa lakini hapa sizungumzii tu Azam, nazungumzia timu zote kwenye ligi kwa sababu kuandaa timu, kujenga timu ni kitu kigumu sana.
"Ni kazi ngumu sana...kazi ngumu kwa wote, makocha, benchi lote la ufundi, na watu wote wanaoizunguka timu na wakati mwingine unajikuta kazi yako yote inaharibiwa kwa sababu uamuzi mmoja tu.

"Sisi sote tunafanya makosa. Ni kawaida, watu tuko hivyo, binadamu tuko hivyo lakini nachotaka kusema ni kwamba tunataka tuchezeshwe  kwa haki,sisi sote, sizungumzii tu Azam,sote hicho ndicho tunataka."