Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aucho afungiwa mechi tatu, kulipa faini Sh500,000

Nyota wa Yanga, Khalid Aucho amefungiwa kutocheza michezo mitatu na faini ya Sh500, 000 (laki tano) kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji Ibrahim Ajibu wa Coastal Union, kwenye mchezo uliofanyika Uwanja wa Mkwakwani,  jijini Tanga, Novemba 8.

Katika mchezo huo, Coastal Union imetozwa Sh1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la wachezaji kuchelewa kutoka nje ya chumba cha kuvalia nguo, jambo lililosababisha mchezo kuchelewa kuanza kupindi cha kwanza na baada ya mapumziko, hivyo kuharibu programu za mrusha matangazo ya runinga (Azam TV) ambaye ni mdhamini mwenye haki za matangazo ya runinga

Aucho atakosa michezo mitatu kuanzia  dhidi ya Mtibwa Sugar Desemba 16, Tabora United Desemba 22 na 26 dhidi ya Kagera Sugar.