Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ASEC yaifungulia Simba njia Caf

Matumaini ya Simba kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kundi B yamezidi kuwa hai baada ya ushindi wa Asec Mimosas ya Ivory Coast wa mabao 3-0 dhidi ya Jwaneng Gallaxy ya Botswana. 

Mabao ya Asec  yamefungwa na Avo Leibe Junior dakika ya 11, Essis Aka 80' na Sakara Wiliam Karamoko dakika ya 90 na kuifanya timu hiyo kutangulia robo fainali nakuisubiri kati ya Simba yenye pointi tano, Jwaneng pointi nne na Wydad pointi tatu na zinahitaji pointi tisa tu.

Hesabu zilikuwa hivi, Simba inahitaji pointi nne katika mechi zake mbili zilizobakia dhidi ya Asec  ugenini na mchezo wa mwisho dhidi Jwaneng Gallaxy nyumbani ili isonge mbele hatua ya robo fainali, hivyo kufikisha pointi tisa.

Hata hivyo, pointi hizo zinaweza kufikiwa na Wydad endapo itashinda mechi zake mbili zilizosalia dhidi ya Asec na Jwaneng lakini Wekundu wa Msimbazi itafuzu kutokana na matokeo mazuri iliyopata dhidi ya wamorocco kwenye mechi zake mbili.

Katika mechi mbili zilizokutana Simba imefungwa na Wydad bao moja huku yenyewe ikishinda mabao mawili na hivyo inaweza ikaamuliwa kwa matokeo hayo yatakayoifaidiaha wekundu hao kama kigezo cha kwanza cha kuamua atakayepita.