Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Anguti Luis atua Coastal Union, kukiwasha Kagame Cup

Muktasari:

  • Beki huyo kutoka nchini Uganda anajiunga na Coastal Union akitokea KCCA ya nchini kwao, na tayari ametambulishwa na klabu hiyo ya jijini Tanga.

Beki Anguti Luis atakuwa sehemu ya kikosi cha Coastal Union msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Beki huyo kutoka nchini Uganda anajiunga na Coastal Union akitokea KCCA ya nchini kwao, na tayari ametambulishwa na klabu hiyo ya jijini Tanga.

Taarifa iliyochapishwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii ya Coastal Union imemmwagia sifa Anguti, ambaye anaaminika anakwenda kuendeleza mazuri katika safu ya ulinzi ya klabu hiyo.

Anguti ana uwezo wa kucheza namba nne na tano ataanza kuonekana akiwa na Coastal Union kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na kati 'CECAFA Kagame Cup' itakayoanza Julai 9, 2024.

Beki wa kati Coastal, Lameck Lawi alitambulishwa kujiunga na Simba, lakini Wagosi wa Kaya waliibuka na kusema dili hilo la uhamisho lilishakufa baada ya Wekundu wa Msimbazi kushindwa kutimiza masharti na hivyo nyota huyo anabaki Tanga.