Amunike amvaa Feisal juu ya kadi

Muktasari:

Tanzania inajianda na mechi ya pili katika Kundi C dhidi ya Kenya itakayochezwa Alhamisi

Cairo, Misri. Kocha Emmanuel Amunike amemshtukia kiungo wake Feisal Salum juu ya kupata kadi nyingi kila anapocheza.

Kiungo Fei Toto alipata kadi ya njano katika mchezo dhidi ya Senegal akiwa moja ya wachezaji wanne wa Tanzania waliopata kadi katika mchezo huo.

Akizungumza leo Amunike amesema amepanga kulifanyia kazi suala la viungo wake kupata kadi nyingi

Amunike alisema tatizo hilo la Feisal ameliona kuanzia mechi za klabu yake ambapo atazungumza naye kumpa ushauri.

Kocha huyo alisema kazi hiyo haitakuwa kwa Feisal pekee na kwamba ataifanya pia kwa viungo wengine kwa kuwa linaweza kuwapa changamoto zaidi mbele.

"Tumeliona hilo hata sisi hatupende kuona wachezaji wetu wanapata sana kadi kuna mambo mengi yanasababisha mtu kupata kadi lakini tunalufanyia kazi," alisema Amunike.

"Hatutaki kuona kila mchezaji wetu anakuwa na kadi nyingi linaweza kutupa ugumu huko mbele na hii imetokea kwa Feisal na viungo wengine tutakaa nao."