Prime
Aliyempiga kocha Mbeya City afungiwa msimu mmoja

KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu imemfungia kocha wa magolikipa wa Mashujaa FC, Shomari Ndizi msimu mzima wa 2023/24 kushiriki michezo yote iliyo chini ya TFF.
Katika taarifa iliyotolewa na bodi hiyo imeeleza adhabu hiyo imetokana na kosa la kumpiga ngumi usoni kocha mkuu wa Mbeya City, Abdallah Mubiru wakati wa mechi ya mtoano kati ya Mbeya City na Mashujaa iliyopigwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Tukio hilo lilitokea wakati Mashujaa wamepata bao na wakaenda kushangilia wakipita benchi la ufundi la Mbeya City ndipo lilipotokea tukio hilo lisilo la kiungwana.
"Amefungiwa kushiriki michezo yote ya Ligi na mashindano yote yaliyo chini ya Shirikisho la Soka (TFF) kwa msimu mzima wa 2023/24 pamoja na kutozwa faini ya Sh2 milioni,"