Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ali Kiba awaweka benchi warembo wanaomtamani

Dar es Salaam. Mke wa Msanii wa muziki wa Bongo Fleva , Ali Kiba, Amina Khalef amesema suala la mumewe kuoa mke wa pili anamuachia Mungu lakini akisema  wanawake ambao wanampenda na wanatamani kuolewa na yeye wasubiri kwa kuwa ana nafasi tatu za kuoa kama ambavyo dini ya Kiislam inavyoruhusu.
 Akizungumza katika kipindi cha Leo Tena, kinachorushwa Redio ya Clouds, awali Amina alionekana kuwa mzito kulijibu swali hilo mpaka pale watangazaji walipombana.
Wakati kwa upande wa Ali Kiba amesema yeye ataoa kama mkewe ataridhia kufanya hivyo na kuongeza kuwa kwa sasa angependa kuwa na huyo tu.
Akihojiwa katika kipindi cha 360 mapema asubuhi leo, Kiba aliwaambiwa wanawake ambao wanampenda na wanatamani kuolewa na yeye wasubiri kwa kuwa ana nafasi tatu za kuoa kama ambavyo dini ya Kiislam inavyoruhusu.
Hata hivyo alivyoulizwa kama nafasi iayofuata ni ya mrembo Jokate Mwegelo, ambaye aliwahi kuwa na mahusiano naye, alikwepa kulijibu hilo na kumtaka mtangazaji Sam waheshimiane kwa kuwa sasa hivi ni mume wa mtu.
Kuhusu chakula ambacho anapenda kumpikia mumewe, Amina  ana elimu ngazi ya shahada katika masuala ya biashara, amesema  ni wali na samaki.
Ali Kiba alifunga ndoa na Amina Aprili 19 mjini Mombasa, na kisha kufanya sherehe nyingine kubwa nchini katika Hoteli ya Movenpick iliyohudhuriwa na watu mbalimbali maarufu akiwemo mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne, mama Salma Kikwete.
Moja ya mambo yaliyovutia katika sherehe hiyo ni pamoja na kurushwa mubashara kwa sherehe hizo Kenya na Tanzania kupitia kituo cha Azam TV tukio ambalo lilikuwa linafuatiliwa na mamilioni ya watu.