Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

AKILI ZA KIJIWENI: Waziri Palamagamba Kabudi kweli Profesa

HAMDI Pict
HAMDI Pict

Muktasari:

  • Hii ni wizara yetu na vitu kama hivyo vya msingi kwa mtu wa michezo kweli hawezi kukubali vimpite maana bajeti ndiyo imeshikilia mafanikio au kuanguka kwa sekta yetu pendwa nchini.

JANA Jumatano, kundi lote hapa kijiweni tulikuwa tumekusanyana kusikia na kuona Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi akisoma hotuba ya makadirio ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

Hii ni wizara yetu na vitu kama hivyo vya msingi kwa mtu wa michezo kweli hawezi kukubali vimpite maana bajeti ndiyo imeshikilia mafanikio au kuanguka kwa sekta yetu pendwa nchini.

Tunavyotamba hii ni wizara ya raha basi ni sababu ya bajeti ya maana na kama raha zikikosekana basi ujue kuna kitu hakipo sawa kwenye upande wa bajeti, hilo liko wazi.

Basi buana Mheshimiwa Kabudi akasoma bajeti moja ya kibabe sana ambayo ni kiasi cha Sh519.66 bilioni ambacho ni kikubwa zaidi katika historia ya wizara hiyo na sababu ya hilo inajulikana ambayo ni kuwezesha kufanikisha maandalizi ya mashindano ya CHAN na AFCON ambayo Tanzania itaandaa pamoja na Kenya na Uganda.

Sasa katika kuchangia hotuba hiyo, mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku akamuomba Waziri Kabudi atoe taarifa ya kilichojadiliwa katika kikao baina yake na klabu za Yanga na Simba pamoja na mamlaka za soka nchini juu ya hatma ya mechi baina ya timu hizo iliyopangwa kuchezwa Machi 8 mwaka huu.

Baadaye Mbunge wa Manonga, Seif Gulamali naye akamuomba Waziri Kabudi abadilishe muundo na uendeshaji wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) akisema kwa sasa ipo chini ya TFF akipendekeza ijitegemee.

Lakini Profesa Kabudi alijibu vizuri hayo ni masuala ambayo kwa mujibu wa kanuni na utaratibu wa uendeshaji wa mchezo wa mpira wa miguu, serikali haiwezi kuyafanya kwa vile haipaswi kuingilia taasisi ambayo inafanya hivyo kwa hapa nchini ambayo ni TFF.

Ni jambo ambalo limetushangaza sana hapa kijiweni kwa vile wakati Profesa Kabudi anateuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, tulimchukulia poa na kuamini siyo mfuatiliaji wa mambo ya kimichezo hasa soka.

Kumbe Kabudi anautumia vyema Uprofesa wake kwa kuwa na ufahamu wa mambo mengi ambayo mengine watu hawamdhanii kama anaweza kuyaelewa vyema kama hilo la taratibu za uendeshaji wa soka.