Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

AKILI ZA KIJIWENI: Simba Queens ikubali kuanza upya

SIMBA Q Pict

Muktasari:

  • Ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake ambao baadhi wameuchukua kwa nyakati tofauti na pia kupata fursa ya kushiriki klabu bingwa Afrika ya wanawake mara moja, ni mambo yanayoonekana yameshawalevya na hawana tena ari ya kuipigania timu hiyo.

KILE kichapo cha bao 1-0 ambacho Simba Queens imekipata kutoka kwa Yanga Princess Jumanne wiki hii kina ujumbe mkubwa kwenda kwa uongozi wa klabu ya Simba juu ya timu yao hiyo ya wanawake.

Ujumbe wenyewe ni kwamba Simba Queens projekti yake ya mafanikio ya kipindi cha takribani miaka mitano iliyopita inaelekea mwishoni na sasa inahitaji maboresho makubwa badala ya kuamini kuwa bado iko vizuri na inatamba katika soka la wanawake nchini.

Hatusemi kwa sababu imefungwa na Yanga Princess kwani hilo ni jambo la kawaida katika soka kwa timu kupoteza, lakini namna ambavyo inapoteza mchezo ndivyo watu tunaweza kupata majibu kwamba ni hali ya kawaida au kuna shida mahali.

Na kwa vile kijiwe hiki hakina mambo ya kuzunguka zunguka na kinapiga pale panapouma, ngoja tuwaambie ukweli Simba ili waweze kuitafutia suluhisho la haraka Simba Queens kama kweli wanataka kuendelea kutamba katika soka la wanawake.

Kwanza timu msimu huu imeshuka kiwango na haichezi vizuri hata kama iliongoza kwa kipindi fulani haina ile floo ya Simba Queens ambayo tumeizoea kuiona hapo nyuma kwamba hata ikifungwa, mpinzani anamaliza mechi akiwa hoi bin taabani.

Lakini kingine inaonekana kuna wachezaji pale wamesharidhika na mafanikio na hakuna kipya ambacho wanaweza kuipatia Simba Queens. Walishajenga utawala wao siku za nyuma na sasa wanaamini hata wakicheza vibaya wataendelea tu kuwepo kwenye timu.

Ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake ambao baadhi wameuchukua kwa nyakati tofauti na pia kupata fursa ya kushiriki klabu bingwa Afrika ya wanawake mara moja, ni mambo yanayoonekana yameshawalevya na hawana tena ari ya kuipigania timu hiyo.

Lakini pia inaonekana hata upande wa utawala, hakuna ule ukaribu na sapoti kubwa kwa timu kama ilivyokuwa zamani hasa ya kifedha na mipango jambo ambalo linasababisha hamasa ya timu ipungue na ianze kupoteza mvuto wake taratibu.

Wahenga walisema usipoziba ufa utajenga ukuta hivyo kama Simba isipochukua tahadhari mapema kuhusu Simba Queens, itapoteza utawala kwa soka la wanawake nchini.