Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ajib si wa kwanza hawa pia walikacha soka

Muktasari:

Ajib hivi karibuni alitikisa vyombo vya habari baada ya kushindwa na TP Mazembe iliyotaka kumsajili baada ya kumaliza mkataba na Yanga

Dar es Salaam.Wakati baadhi ya wadau wa soka wakishangazwa na kitendo cha Ibrahim Ajib kugomea dili la kucheza TP Mazembe, mshambuliaji huyo inaelezwa kwamba anapitia nyayo walizopita kaka zake hawa.

Iko hivi, Ajib hivi karibuni alitikisa vyombo vya habari baada ya kushindwa na TP Mazembe iliyotaka kumsajili baada ya kumaliza mkataba na Yanga.

Nyota huyo aliyejiunga Yanga akitokea Simba aliwashangaza wengi kwa kitendo hicho, lakini katika soka la Bongo, Ajib si wa kwanza kufanya hivyo.

Mrisho Ngassa

Winga huyu wa Yanga alipata dili la kujiunga na Al-Merreikh ya Sudan, Desemba 2012, lakini aligoma.

Ngassa alipata dili hilo akiwa Azam ambako alikuwa akicheza baada ya Simba kumpeleka kwa mkopo. Hata hivyo, winga huyo alishindwana na Al-Merreikh kabla ya kujiunga na timu kadhaa kisha kurudi Yanga ambako anacheza sasa.

Haruna Moshi (Boban)

Mchezaji huyu ni tofauti kidogo na Ajib, yeye alisajiliwa na kucheza soka la kulipwa nchini Sweden kwenye timu ya Gefle IF, lakini hakudumu na kurejea nchini ambako alijiunga na Simba na kuzunguka timu mbalimbali ikiwamo African Lyon, na sasa Yanga akiwa na mkataba wa miezi sita uliokwisha.

Jeryson Tegete

Nyota huyu wa zamani wa Yanga yeye alipata timu nchini msimu wa 2009, 2010 aliporudishwa Tanzania akitokea Sweden kwenye majaribio aliyokuwa anaelekea kufanikiwa.

Baba yake mzazi, John Tegete alidai mchezaji huyo akiwa Sweden kwenye majaribio alirudishwa haraka viongozi wake wakasema ametoroshwa ili asicheze mechi ya Yanga na Simba, ikabidi arudi, kisha wamemtelekeza amekwisha.

Tegete aliachwa na Yanga wakati Hans van der Pluijm akiwa kocha wa timu hiyo, baadae Tegete alijiunga na Mwadui FC iliyokuwa ikinolewa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.

Nadir Haroub (Canavaro)

Beki huyo kisiki wa zamani wa Yanga na Taifa Stars pia aliwahi kugomea dili la kujiunga na timu ya Vancouver WhiteCaps ya Canada.

Nahodha huyo wa zamani aligoma kuichezea timu hiyo akimuacha mchezaji mwenzake, Nizar Khalfan aliyetokea Moro United akikomaa kwenye timu hiyo.

Canavaro alirejea Yanga ambako aliendelea kucheza Yanga hadi alipostaafu na sasa ni meneja.

Victor Costa 'Nyumba'

Beki huyu wa zamani wa Simba naye hakuwa na maisha mazuri ya soka nje ya nchi baada ya kupata timu Afrika Kusini ambako alikwenda lakini baada ya muda Simba ikamrudisha.

Costa pia alipata timu Msumbiji, Simba ikamrudisha tena lakini baada ya muda ikamuacha na soka lake likaishia hapo.

Edibily Lunyamila

Winga machachari aliyetingisha Afrika Mashariki na Kati kutokana na uwezo aliokuwa nao mwaka 1995, alipata nafasi ya kwenda Ujerumani kucheza soka la kulipwa akitokea Yanga lakini viongozi wa timu hiyo walimkatili kwa kumrudisha Taanzania akiwa kwenye majaribio yaliyokuwa yanaelekea kufanikiwa kwa ajili ya kuja kucheza na Simba kwenye mechi ya Kombe la Hedex.

Mbali na wachezaji hao kushindwa kumudu kucheza soka la nje ya nchi, lakini wapo wenzao ambao walikomaa akiwamo Danny Mrwanda, Abdi Kassim 'Babi', Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta, Simon Msuva, Farid Mussa na Shaban Chilunda.