Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Adam aitanguliza JKT Tanzania

Muktasari:

Safu ya kiungo ya Simba alikuwepo Jonas Mkude, Gerson Fraga ambao walionekana kushindana vyema na viungo wa JKT ambao walikuwa watatu Mwinyi Kazimoto, Hafidhi Mussa na Nurdin Mohammed.

BAO la dakika 24, lililofungwa na mshambuliaji wa JKT Tanzania  Adam Adam, lilitosha kuitanguliza timu yake dhidi ya mabingwa watetezi Simba katika mechi ya Ligi Kuu Bara inayoendelea jioni hii Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

JKT Tanzania walionekana kucheza vyema na kwa nidhamu kubwa katika kushambulia na kukaba dhidi ya wapinzani wao.

JKT Tanzania walikuwa wakitumia mipira mirefu kushambulia kupitia kushoto na kulia huku mastraika Adam na Daniel Lyanga, wakiongoza safu ya ushambuliaji ya timu yao.

Simba wao walikuwa wakionekana kufanya makosa hasa kuanzia safu ya ulinzi kwa kuwaacha washambuliaji wa JKT Tanzania Lyanga na Adam  ambaye baadae alifunga bao.

Safu ya kiungo ya Simba alikuwepo Jonas Mkude, Gerson Fraga ambao walionekana kushindana vyema na viungo wa JKT ambao walikuwa watatu Mwinyi Kazimoto, Hafidhi Mussa na Nurdin Mohammed.

Eneo hilo la kiungo la timu zote mbili lilionekana kuwa na ushindani mkubwa kwani muda mwingi mpira ulikuwa ukichezwa hapo.

Simba walikuwa na mapungufu safu ya ushambuliaji pengine ndio ilifanya kushindwa kupata bao kipindi cha kwanza.

Mapungufu hayo ya Simba yalionekana kupata shida kucheza na mshambuliaji mmoja Meddie Kagere ambaye muda mwingi walinzi wa JKT walimkaba.

Nyuma ya Kagere alikuwepo Ibrahim  Ajibu ambaye alikuwa akicheza mbali na straika mwenzake na muda mwingi alionekana kufata mipira nyuma na pembeni na hata baadhi ya pasi alikuwa akipoteza.

Katika eneo la mawinga Simba walikuwa na Shiza Kichuya ambaye alionekana kupoteza mipira na hata krosi alizokuwa akipiga nyingi zilishindwa kuwa na hatari kwa maana kwenda kwa washambuluaji.

Huenda Kichuya alishindwa kufanya vizuri kutokana na kukosa ufiti wa mechi huku winga mwenzake Luis Miquissone alionekana kucheza vyema kwa maana ya kushuka chini kusaidia kukaba na hata kuanzisha mashambulizi.

Luis mbali ya kutimiza majukumu hayo alionesha uwezo kumiliki mpira kwa maana ya kupiga chenga wachezaji wa timu pinzani mpaka mashabiki waliokuwa uwanjani kumpigia makofi ya kumpongeza na kupiga pasi nyingi ambazo zilifika kwa walengwa.