#UCHAGUZI SIMBA: Kaduguda agomea wapiga kura, polisi wamtoa nje

Muktasari:

Idadi ya wapiga kura waliotangazwa ambao ni 1728 tofauti na iliyotajwa awali ya 1720, ambapo kabla ilikuwa 1486.

Dar es Salaam. Mgombea ujumbe wa Simba, Mwina Kaduguda amechafua hali ya hewa baada ya kugomea idadi ya wapiga kura.

Kaduguda ameongozana na wajumbe wenzake kilio chake ni juu ya idadi ya wapiga kura waliotangazwa ambao ni 1728 tofauti na iliyotajwa awali ya 1720, ambapo kabla ilikuwa 1486.

Amesema kuongezeka kwa wapiga kwa kiwango kikubwa kwa haraka ni jambo lisilowezekana.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba, Boniface Lyamwike ametoa muuongozo kwa wapiga kura muda mfupi kabla ya zoezi la kupiga kura kwenye Uchaguzi mkuu wa Simba kuanza.

Alisema wapigakura wataraliwa kuchagua wajumbe watano pekee kati ya wagombea 17 na sheria inasema mmoja kati yao lazima awe mwanamke

"Mtapewa Fomu mbili mkononi, moja ya Mwenyekiti (mgombea mmoja) na nyingine ya wajumbe."

Alisema zoezi la kuhesabu kura ni la kamati na hawatoruhusu mtu yoyote kuwasaidia.

Alisema mgombea ndiye anayeujua uchungu wa nafasi anayoigombea, hivyo yeye ndiye atasimamia kura zake au mtu anayemuamini {wakala)

Alisema baada ya kupiga kura mwanachama atatoka nje na hatoruhusiwa kurudi ndani na watakaopiga kura ni wanachama 1728.