Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tujitokeze Uwanja wa Taifa kwa wingi kuitia nguvu Serengeti Boys

Muktasari:

  • Hilo ni pambano la nusu fainali ya michuano hiyo, ambayo Serengeti Boys wanaitumia kama sehemu ya kujiweka sawa kabla ya kushiriki fainali hizo za Afcon mwakani wakiwa kama wenyeji.

MASHUJAA wa Tanzania katika michuano ya mchujo kuwania ushiriki wa Fainali za AFCON kwa Vijana U17 kwa mwaka 2019 Kanda ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Serengeti Boys, leo Ijumaa inavaana na vijana wenzao wa Uganda.

Hilo ni pambano la nusu fainali ya michuano hiyo, ambayo Serengeti Boys wanaitumia kama sehemu ya kujiweka sawa kabla ya kushiriki fainali hizo za Afcon mwakani wakiwa kama wenyeji.

Hata hivyo, hiyo haifanyi mechi hiyo dhidi ya Uganda kuchukuliwa kama mechi ndogo ama ya kuchukuliwa poa. Ni mechi muhimu kwa vijana wetu na kipimo kizuri kwa timu hiyo katika kujiandaa na uenyeji wa fainali za za Afrika.

Uganda waliomaliza nafasi ya pili katika Kundi B ni moja ya timu ngumu na yenye kuundwa na wachezaji wenye miili mikubwa na wanacheza soka la nguvu, hivyo mechi hiyo inaweza kuwa kipimo kizuri kwa vijana wetu katika maandalizi yao.

Serengeti imekuwa kivutio kwa mashabiki wa soka kwa uwezo na vipaji vya wachezaji wa timu hiyo katika mechi zao za Kundi A walioliongoza bila kupoteza mchezo wowote, wakiwazidi Rwanda waliomaliza wa pili ambao leo wataumana na vinara wa Kundi B, Ethiopia iliyo tishio kubwa katika michuano hiyo.

Bahati nzuri Kocha Mkuu wa timu hiyo, Oscar Milambo ameweka bayana kwamba hawana cha kupoteza katika michuano hiyo kwa vile tiketi ya mwakani wanayo, lakini kila mechi wanayocheza wanaifanya kama fainali ili kuwajenga vijana wake.

Kwa hakika kocha huyo wala haongopi kwani tangu walipoanza kuvaana na Burundi na kushinda mabao 2-1, Serengeti haijapoa kwa kugawa dozi za maana kwa wapinzani wao wakiwamo Rwanda waliofumuliwa mabao 4-0.

Inawezekana wengi wakaona Serengeti ilipata ulaini kwa wapinzani wao wa Rwanda kwa vile tayari kila mmoja alishafuzu, lakini mechi ya leo dhidi ya Uganda ndio kipimo sahihi ch kuonyesha kuiva kwa vijana wetu kwa ajili ya Afcon 2019. Hivyo katika kuhakikisha vijana wetu wanaendelea kutupa raha na kutupunguzia machungu ya kuchemsha kwa wawakilishi wetu wengine katika michuano ya kimataifa, ni vyema mashabiki wakajitokeza kwa wingi viwanjani kuwatia nguvu.

Kila shabiki mwenye nafasi anapaswa kujitokeza Uwanja wa Taifa kwa nia ya kuwapa nguvu vijana kuweza kupata matokeo mazuri mbele ya Uganda na kutinga fainali.

Ushindi wowote kwa vijana hao utasaidia kuwaongezea kujiamini na kuiwakilisha vyema Tanzania katika fainali za Afcon ambazo kama nchi tutashiriki kwa mara ya pili mfululizo baada ya mwaka jana zilipofanyika Gabon.

Kujiamini kwa vijana kutasaidia kufanya uenyeji wetu uwe na tija na kuifanya michuano hiyo inoge. Ndio, mwenyeji wa michuano kutolewa mapema hupunguza hamasa na amshaamsha viwanjani, ndio maana tunapenda Serengeti waendelee kupata matokeo mazuri kufanya mashabiki kuwa na kiu nao.

Asilimia kubwa la wapenzi na mashabiki wa soka wanaipenda Serengeti Boys na kuwa na hamu siku zijazo kama vijana wake wataendelea kutunzwa waje kuwa Taifa Stars ya baadaye na kuendeleza moto wake ule ule.

Kwanini mashabiki wanaipenda Serengeti? Ni kwa sababu ya matokeo mazuri inayopata ambayo kwa timu ya wakubwa imekuwa muhali, kiasi cha kupunguza mapenzi kwa timu hiyo. Hii ni kuonyesha matokeo mazuri kwa timu zetu ni moja ya sababu ya kuwavutia mashabiki kuzipenda na kuzifuatilia timu zao kwa ukaribu kama wanavyofanya sasa kwa Serengeti, hata kama ni kweli viingilio vya kuiona michuano hiyo ya CAF-Cecafa haipo na watu kufurika uwanjani.

Serengeti iliyopita iliwafanya mashabiki wengi kuhudhuria kwa wingi uwanjani kuiangalia ikipepetuana katika mechi zao kwa sababu ilikuwa ikipata matokeo mazuri. Hata timu ya sasa imepita na kufuata nyayo hizo hizo na ndio maana tunaendelea kuwasisitizia vijana wetu wafanye kweli mbele ya Uganda ili wazidi kuungwa mkono na pia kujijengea ari ya kujiamini na kutuwakilisha vyema.

Muhimu zaidi ni kwa vijana hao watambue kuwa Watanzania wapo nyuma yao na

wajibu wao kutowaangusha kwa kuhakikisha wanainyoosha Uganda kisha kusubiri kujua watacheza na Ethiopia ama Rwanda tena katika fainali Jumapili hii.

Kila la heri Serengeti Boys, tuendeleeni kuiunga mkono kwa kujitokeza kwa wingi uwanjani.