Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simiyu aisaka rekodi London 7s

Muktasari:

  •  Kenya wanahitaji  alama saba kufikisha alama 100 za dhahabu katika historia ya michezo hiyo

Nairobi. Saachache kabla Kenya haijajitosa uwanjani kukabiliana na Marekani katika mchezo wao wa kwanza wa mashindano ya London 7s, Kocha Innocent Simiyu ameapa kuandikisha historia Jijini London.

Akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kipyenga cha kwanza cha mashindano ya London 7s, ambayo ni mkondo wa tisa kati ya misururu 10, ya msimu wa 2017/18 ya kombe la Raga, maarufu kama HSBC World Rugby Sevens Series, Simiyu amesema anataka kufanya jambo kubwa kwenye michezo hiyo.

Wakiwa wamesalia na alama saba kufikisha alama 100 za dhahabu katika historia ya michezo hiyo, Kenya imejipanga kuhakikisha London 7s inakuwa ni sehemu ya kuweka rekodi hiyo na kwa kuanzia, Simiyu ameapa lazima Marekani wale za uso.

Alama za juu ambazo Kenya imewahi kufikisha katika historia ya mchezo huo, ni alama 99, iliyoandikisha katika msimu wa 2012/2013, lakini tangu hapo, wamekuwa wakihangaika kuvuka alama hizo bila mafanikio na Simiyu anataka kuwa kocha wa kwanza kuandikisha alama zaidi ya hapo.

Msimu huu, Shujaa 7s wanahitaji kutinga hatua ya robo fainali tu ili kufanikisha malengo hayo. Wakiingia hatua hiyo, alama za chini ambazo wa uhakika kuzikusanya ni alama 10 ambazo zinawatosha kabisa.

Kama watashindwa kutinga robo fainali ya taji kuu, basi watahitaji kutinga fainali ya Kombe la Challenge. Hii itawahakikishia kuzoa alama saba kama watapoteza kwenye fainali na alama nane wakishinda.

Kenya wanaingia dimbani katiia mchezo wa kwanza dhidi ya Marekani inayonolewa na Mkenya Mike Friday (7.42 mchana), kabla ya kuwavaa Ufaransa kuanzia saa 10.48 alasiri. Baadae watahitimisha mechi za makundi kwa kukwaana na wenyeji England (2.16 usiku).

Itawakosa Ouma na Oliech

Kenya itawakosa nyota wake wawili tegemeo, Oscar Ouma na Sammy Oliech.

Hata hivyo, habari njema ni kwamba, Oscar Oyodi anarejea kikosini baada ya kukaa nje kwa miezi mitatu akiuguza jeraha. Deniss Ombachi ambaye alitazamiwa kurejea baada ya kukaa nje kwa muda mrefu ameachwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Raga nchini KRU, ni kwamba nyota huyo, ambaye mara ya mwisho kuonekana uwanjani ilikuwa ni mwaka 2017 kwenye msururu wa Dubai 7s, hatokuwa katika kikosi cha Simiyu kutokana 'sababu binafsi'. Nafasi yake imechukuliwa na kinda anayekuja kwa kasi, Eric Ombassa.