Simba wajifua usiku, Chama ndani

Monday January 17 2022
Simba kuj PIC
By Saddam Sadick

Mbeya. Licha ya kukutana na ratiba ngumu, lakini kikosi cha Simba chini ya Kocha Mkuu, Pablo Franco kimepambana na kutumia dakika 45 kujifua kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Mbeya City.

Timu hiyo iliwasili jijini hapa na kwenda moja kwa moja katika Hotel ambapo leo jioni ilikuwa ifanye mazoezi lakini ilikutana na ratiba ngumu muda huo kutokana na kuwepo kwa Championship baina ya Ken Gold na Pan Africa.

Hata hivyo bingwa huyo mtetezi aliamua kukomaa kusubiri mchezo huo kumalizika na kuanza mazoezi saa 12:10 hadi saa 1:05 usiku.

Katika mazoezi hayo ilishuhudiwa kiungo na kipenzi cha mashabiki, Clatous Chama akiwa miongoni mwa nyota wa timu hiyo waliojifua tayari kuwakabili Mbeya City mchezo utakaopigwa kesho Jumatatu katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Mazoezi hayo  yalijikita katika kufunga mabao kama alivyoahidi mapema Kocha Franco kuwa watashuka uwanjani wakishambulia zaidi kusaka mabao, lakini pia kupiga pasi na kukaba.

Advertisement