Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba ni Banda tu!

Banda aitanguliza Simba

KIKOSI cha Simba wapo visiwani Zanzibar wakiwa kamili gado isipokuwa winga wake, Mmalawi, Peter Banda aliyepo kwenye majukumu ya timu yake ya taifa ya Malawi inayoshiriki Fainali za Afcon, zinazofanyikia Cameroon.

Mratibu wa klabu hiyo, Abbas Ally Suleiman alisema ni Banda pekee ndiye atakayekosekana kwenye kikosi cha Simba ambayo imepangwa Kundi C na timu za Salem View na Mlandege na itaanza mechi zake keshokutwa Jumatano dhidi ya Salem View mechi ikipigwa saa 10:15 jioni kwenye Uwanja wa Amaan katika michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Mratibu huyo pia alisema hajapata taarifa zozote za kuwepo kwa wachezaji wapya watakaowatumia kwenye michuano hiyo, licha ya ukweli Mwanaspoi lilipenyezewa kuwa nyota wawili kutoka Afrika Magharibi.

“Hakuna taarifa za mchezaji mpya yeyote wala yule ambaye atakuja katika majaribio, ila ninachojua ni kwamba timu inaondoka huko Dar es Salaam bila ya Banda tu, hilo la wageni kutoka nje ya nchi, labda litokee tukishafika Zanzibar,” alisema Ally.

Naye Kocha wa Simba, Pablo Franco alisema kikosi chake kinahitaji ubingwa wa michuano hiyo, kwani itasaidia kujenga morali kwa wachezaji wake itakaporejea katika ligi na michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Pablo alisema malengo ya Simba ni kufanya vizuri katika kila shindano ambalo watakuwepo na hilo ndio wamepanga kwenda kulifanya huko Zanzibar kutwaa ubingwa wa kombe hilo.

“Msimu uliopita tulilikosa baada ya kupoteza mechi ya fainali kwahiyo msimu huu tumepanga kuonyesha ukubwa wa Simba kutwaa taji hilo na kuongeza idadi ya mafanikio,” alisema Franco na kuongeza;

“Kuna baadhi ya wachezaji hawakutumika zaidi kwenye ligi watapata nafasi ya kucheza katika mashindano haya, pia tunaweza kuona sura mpya.”