‘Shetani Yanga’ aibukia kwa Mkapa-VIDEO
Dar es Salaam. Shabiki wa Yanga, Idrisa Zakaria 'shetani wa Yanga’ ameibuka kwa Mkapa kwa staili ya kitofauti ambayo amesema ni ya utabiri wa kipigo kwa Simba.
Yanga itakuwa mgeni kwenye dabi hiyo ya kwanza ya Ligi Kuu ya NBC msimu 2021/22 itakayochezwa saa 11:00 jioni kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa.
'Shetani wa Yanga' ambaye ameibuka kwa Mkapa na staili ya kitofauti amevaa mapembe kichwani, kucha ndefu na kiuononi kajifunga plastiki amesema hiyo ni ishara njema kwa timu yake.
"Staili hii haiwezi kumuacha salama mnyama, natabiri kipindi cha kwanza itakuwa sare ila cha pili, Simba wasubiri tu kitakachowatokea".