Simba, Yanga zatajwa Congo

MMADAGASCAR Randriamanantena Heritiana ambaye anacheza soka la kulipwa visiwani Ngazija huko Comoro, ameuzungumzia mchezo wa Simba dhidi ya Yanga utakaopigwa kesho kwenye Uwanja wa Mkapa kwa kusema ni kati ya dabi zenye msisimko zaidi Afrika kutokana na mvuto wake.
Beki huyo wa kushoto ambaye anaichezea Volkano FC, alisema kwa mtazamo wake dabi ya Simba na Yanga inaweza kushika nafasi ya tatu Afrika kwa ubora kwenye orodha yake nyuma ya Cairo Dabi kati ya Al Ahly na Zamalek, Soweto Dabi kati ya Kaizer Chiefs na Orlando Pirates na Casablanca Dabi kati ya Raja Casablanca na Wydad Casablanca.
Heritiana alisema, “Yanga na Simba nimeanza kuzisikia miaka mingi sana, ni timu kubwa za Tanzania ambazo zimekuwa na ushindani mkubwa. Kuna kipindi niliwahi kupata ofa ya kuja kufanya majaribio lakini sikuvutiwa na hilo kwa sababu sikuwa najiweka kwenye daraja la kufanyiwa majaribio ndio maana nikakataa mualiko wao.
“Sidhani kama kuna dabi nyingine kubwa zaidi ya Simba na Yanga kama ukiziondoa, Cairo dabi, Soweto dabi na Casablanca dabi, natamani siku moja nije kuishuhudia.”