Sawadogo hakuwa na maisha marefu Simba

Muktasari:
- Maisha ya kiungo huyo Msimbazi yalianza kuonekana si marefu mapema sana tofauti na mashabiki walivyotegemea, kutokupata nafasi kwake kwenye kikosi cha kwanza kuliashiria huenda panga la Simba kupita kwake muda wowote baada ya msimu kumalizika
Kama kuna kitu mashabiki wa Simba mitandaonj wanaulizia ni Thank You ya kiungo mkabaji Ismael Sawadogo, na sababu kubwa ni kiwango kidogo alichokionyesha kiungo huyo.
Maisha ya kiungo huyo Msimbazi yalianza kuonekana si marefu mapema sana tofauti na mashabiki walivyotegemea, kutokupata nafasi kwake kwenye kikosi cha kwanza kuliashiria huenda panga la Simba kupita kwake muda wowote baada ya msimu kumalizika
Hatimaye panga la Simba limepita kwa kiungo Sawadogo aliyesajiliwa dirisha dogo la usajili msimu uliopita wa 2022/23.
Alitajwa kuwa mbadala wa kiungo mahiri, Jonas Mkude, alianza akionekana anaweza kubadilika kadri muda unavyokwenda lakini baada ya kucheza michezo kadhaa, maji na mafuta yalijitenga akakosa nafasi kikosi cha kwanza kwa kuonekana hana uwezo.
Lakini pia aliathiriwa na kutocheza muda mrefu huko nyuma.
Kiungo huyo mkataba wake ambao alisaini na Simba na ili mkataba uvunjwe aliwataka kulimpa kitita cha dola laki 3, ambayo ni sawa na Sh718 million, lakini kama Simba wakinuuliza timu inayomtaka ilipe dola laki 6, zaidi ya Sh1.4 bilioni
Sawadogo ambaye alisajiliwa kwa mbwembwe nyingi, amewahi kuzitumikia klabu kadhaa barani Afrika ikiwemo ENPPI ya Misri, US Ouagadougo, pamoja El Jadida ya Morroco.