Nabi awatuliza mashabiki Yanga

Saturday May 14 2022
watuliza pic
By Ramadhan Hassan

Dodoma. Kocha mkuu wa Yanga, Nesreddine Nabi amewatuliza mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia ubingwa upo pale pale kinachotakiwa ni kuendelea kuwapa ushirikiano wachezaji.

Yanga inashuka dimbani kesho saa 10 jioni kucheza dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo wa Ligi kuu unaotarajiwa kufanyika katika uwanja wa Jamhuri.

Yanga inahitaji ushindi katika mchezo huo ili kuongeza gepu la pointi dhidi ya Simba ikiwa ni sehemu ya mbio za ubingwa msimu huu

Timu hiyo  inaongoza Ligi ikiwa na pointi 57 huku Dodoma Jiji wao wakiwa  nafasi ya nane na pointi 28 ambapo mechi iliyopita dhidi ya Polisi Tanzania walitoka suluhu ugenini dhidi ya Polisi Tanzania mjini Moshi.

Kocha huyo amewatuliza kwa kuwataka kutulia kwani mambo mazuri yanakuja na timu hiyo itaanza kupata ushindi katika mchezo wa kesho dhidi ya Dodoma Jiji.

“Lakini wanapaswa kujua sisi kama walimu hivyo ni vitu vya kawaida.Kuna wakati tunapaswa kuangalia mbele tunaamini hakuna haja ya kupaniki  leo tupo mbele tuna gape ya pointi nane ni  nyingi sana

Advertisement

Amesema Mashabiki wajue kuna kipindi mambo hayaendi vizuri kinachotakiwa ni kuendelea kuwaamini wachezaji  ili wafanye vizuri.

“Tokea mwanzo wa msimu wamekupa furaha na unatembea kifua mbele, unavimba unavaa jezi siku saba sasa wale wachezaji wanapitia wakati mgumu wanakosa  sapoti, wanajua  hizi mechi tatu hatutajafanya vizuri,” amesema.

Kocha Nabi amesema watahakikisha wanabeba ubingwa wa Ligi hiyo na ni jambo la muda tu litafika.

Advertisement