Nabi atuliza mzuka Yanga

Friday September 10 2021
Nabi pc
By Thobias Sebastian

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Simba, John Bocco amezidi kuwa bora kwa nyota wa kigeni katika ufungaji licha ya kuwa majeruhi kwa muda.

Zimebaki siku tatu kabla ya wawakilishi wa Tanzania katika Ligi ya mabingwa Afrika, Yanga kucheza mechi ya mkondo wa kwanza dhidi ya Rivers United, Jumapili katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kocha wa Yanga, Nabi Nasreddine alisema kutokana na changamoto mbalimbali ambazo wamezipata wakati wa maandalizi anaimani kubwa watapa ushindi katika pambano hilo ili kurahisisha kazi katika mechi ya marudiano.

Nabi alisema kama ilivyo kawaida alitenga muda wa kutosha kuwafuatilia Rivers na kuona mambo mengi kutoka kwao jinsi ambavyo wanashambulia na kuzuia.

Alisema baada ya kuyaona hayo amerudi katika uwanja wa mazoezi licha ya kushindwa kuwa na wachezaji wote kwa ajili ya kuivaa Rivers na kuwapa mbinu za kutosha.

“Nikuhakikishie hatukuwa na maandalizi mazuri kule Morocco pamoja na wachezaji wetu baadhi hatukuwa nao kwa pamoja kutokana na kuwepo katika majukumu ya timu zao za taifa, lakini mechi hiyo tunashinda.

Advertisement

“Wachezaji waliorudi kutoka katika timu za taifa wote wapo vizuri na nitawatumia, ambao watakosekana kwa sababu mbalimbali kuna mbadala wao watacheza kwenye nafasi hizo.

“Nimewajengea hali ya kujiamini wachezaji wangu pamoja na kuwapa mbinu sahihi ya kupata ushindi ili kujirahisishia kazi katika mchezo wa marudiano, kwani tunacheza na timu ngumu ambayo tunaiheshimu kutokana na ukubwa wao,” alisema Nabi.

Katika hatua nyingine, Nabi alisema wachezaji aliobaki nao ambao hawakuwa katika majukumu ya timu za taifa wengi wamefanya mazoezi kwa ubora na hali ya juu katika kutimiza majukumu yao.


Advertisement