Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkomola ajazwa madini ya Drogba

UNAAMBIWA Kocha wa kikosi B cha Vorskla Poltava, Vitaliy Kosovskyi amempa somo mshambuliaji kinda wa Kitanzania, Yohana Mkomola namna ya kutumia mabavu na akili kama nyota wa zamani wa Chelsea na timu ya Taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba.

Mkomola ambaye yupo nchini Ukraine, alisema amekuwa akifanya mazoezi kwa nguvu kujiweka fiti na wala hakuwa akifahamu nini kocha huyo alikuwa akilenga hadi hapo alipomwuliza na kumweleza kuwa, anatamani kumwona akitumia vizuri nguvu alizonazo.

Kosovskyi ambaye ni mchezaji wa zamani wa Dynamo Kyiv, amekuwa akimfunga kamba yenye mpira unaovutika kiunoni mshambuliaji huyo na kumtaka kumiliki mipira ambayo alikuwa akimpigia mguuni, kifuani na kichwani.

“Huwa napenda kujua umuhimu wa aina ya mazoezi ninayofanya, hupendi kuwa kama Drogba, nikamwuliza kivipi, alikuwa na uwezo wa kufanya lolote hata mbele ya mabeki watatu au wawili, mazoezi haya yatakusaidia,” alisema Mkomola ambaye aliwahi kuichezea Yanga.

Aliendelea: “Nilijisikia vizuri kwa sababu hakuna mshambuliaji ambaye hapendi kuwa kama Drogba, alikuwa akiwasumbua mabeki wakubwa kumzuia ilikua ni kazi.”

Mkomola alisema kocha huyo amekuwa akimkubali kutokana na kujituma mazoezini na anadai kuwa aliwahi kumweleza kuwa kama akiendelea kujituma anaweza kumwombea nafasi ya kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha Vorskla Poltava.

Vorskla Poltava wanashiriki Ligi Kuu Ukraine hivyo hiyo itakuwa ni fursa kwa Mkomola kuonyesha uwezo wake mbele ya Yuriy Maksimov, anayekinoa kikosi cha kwanza.