Metacha: Kwa Diarra tunasubiri

Sunday November 28 2021
Diarra PIC

Golikipa wa Yanga Djigui Diarra.

By Charity James

KIPA aliyewahi kung’ara na Yanga, Metacha Mnata amekiri kwamba hata kama bado angekuwa klabuni hapo, kwa ubora wa Djigui Diarra mwenyewe angeenda benchi.

Metacha ambaye kwasasa anakipiga na Polisi Tanzania alitamba na Yanga kwa misimu kadhaa kabla ya kuondoka kwa sababu mbalimbali ikiwemo kutofautiana na mashabiki wa klabu hiyo.

Diarra amejiunga Yanga msimu huu huku makipa wazawa waliowahi kupita Yanga wakimtaja kuwa ni kipa namba moja Afrika amekuja Ligi kuu kutoa somo wanakitu cha kujifunza kutoka kwake.

Metacha alisema Diarra ni chaguo sahihi Yanga kwa sasa kutokana na ubora alionao na kusisitiza kuwa amekuwa chachu kwao kujifunza kitu kutoka kwake ili na wao waweze kuwa bora zaidi ya walipo sasa.

“Kwenye bora acha iwe bora Diarra ni bora na sio Tanzania tu bali ni Afrika sitaki kuonyesha utofauti wangu na wake ninachoweza kusema ni kipa mzuri na anakitu tunahitaji kujifunza kupitia yeye,”alisema na kuongeza kuwa;

“Ujio wake kwenye ligi ya Tanzania ni mzuri amekuja kipindi sahihi kuchukua nafasi yangu Yanga sina pingamizi wamefanya chaguo sahihi kwa wakati sahii nampongeza kwa kuanza vizuri na tunatarajia mazuri zaidi kutoka kwake,” alisema.

Advertisement

Naye Deo Munishi ‘Dida’ aliyewahi kuwa namba moja Simba, Yanga, Ashanti United na Taifa Stars, alisema wanakitu cha kujifunza kutoka kwa Diarra ni kipa ambaye anaonekana ameanza kucheza ndani kabla hajawa kipa kutokana na namna ya uanzishaji wa mashambulizi kuanzia langoni kwake na kupanga mabeki wake.

“Diarra anajiamini anajua kucheza na miguu zaidi kuliko mikono akiwa golini naamini hadi mabeki zake wanacheza kwa kujiamini kutoikana na umakini na ubora wake awapo langoni, kwa namna anavyocheza inaonekana alikuwa mchezaji wa ndani anajua kuuchezea mpira mguuni anaanzisha mashambulizi akiwa huru kuanzia eneo lake.

Advertisement