Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa wote Yanga waapa

Mastaa wote Yanga waapa

YANGA inaendelea kujifua kujiandaa na mechi yao ijayo dhidi ya KMC, huku kocha mkuu wake, Nasreddine Nabi akiwapiga mkwara mastaa wake kuwa, katika mechi 13 zilizosalia za Ligi Kuu hataki wapoteze pointi na mastaa hao kuapa watafanya kweli kubeba ndoo.

 Katika mechi 15 za duru la kwanza, Yanga ilipoteza pointi sita kutokana na sare tatu, jambo lililomkera Nabi na kusema katika mechi za duru la pili asingependa kuona timu inapoteza pointi.

Kocha huyo raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Tunisia, aliliambia Mwanaspoti kwamba, amefanya kikao na wachezaji pamoja na wasaidizi wake katika benchi la ufundi pamoja na baadhi ya viongozi na kuweka mikakati duru hili.

Nabi alisema wamekubaliana kuzidi kushikamana kwa manufaa ya timu hiyo, lakini akiwataka wachezaji wake kupambana na kutokubali kirahisi kupoteza pointi kwani hataki yatokee ya duru la kwanza walivyopoteza pointi sita.

Yanga ilitoka sare dhidi ya Namungo, Simba na Mbeya City na Nabi alisema hataki wapoteze tena kama ikitokea wamezitema pointi basi zisifikie au kuzidi zile za duru la kwanza, kwani ndizo zilizowakwamisha kuwaacha mbali wapinzani wao kwenye msimamo.

“Bahati nzuri wachezaji wote wameahidi kupambana na tumeanza duru la pili kwa kushinda michezo miwili ya mwanzo, imani yangu hali itakuwa hivyo hadi mwisho wa msimu na kutimiza malengo ya kubeba ubingwa wa ligi tulioukosa kwa misimu minne mfululizo.’

“Nimewaambia wachezaji hatupaswi kuangalia mwenendo ya timu nyingine, ili kujiwekea mazingira ya amani zaidi za kukusanya pointi nyingi na kuweka pengo kubwa zaidi kuliko ilivyo sasa,” alisema Nabi.

Yanga imeiacha Simba kwa pointi nane baada ya kila moja kucheza mechi 17, ikiongoza msimamo na alama 45, huku Simba ikiwa na 37 nyuma yao.

“Kwa kiu ya mafanikio waliyo nayo wachezaji na kikosi kizima kwa ujumla, ninaamini hilo linawezekana msimu huu tutamaliza tukifikia lengo la kubeba ubingwa,” alisisitiza Nabi.

Hata hivyo, ili kufanikisha jambo hilo, Yanga inapaswa kupata matokeo mazuri katika mechi zinazoonekana ngumu ikiwamo dhidi ya Simba, Azam, Namungo, Polisi na KMC za Dar na tatu za ugenini dhidi ya Dodoma Jiji, Biashara United na Mbeya City.