Mashabiki:Tunaitaka Yanga

Mashabiki:Tunaitaka Yanga

Muktasari:

  • Mchezo huo wa Ligi Kuu utapigwa uwanja wa Majimaji mjini Songea, ambapo KMC ndio wenyeji.

Songea. Usiku? Tunaitaka Yanga. Ni sauti za baadhi ya mashabiki ambao walikuwa wamepanga foleni katika uwanja wa Majimaji mjini hapa tayari kushuhudia mchezo wa Ligi Kuu kati ya  KMC na Yanga.

Mchezo baina ya timu hizo unatarajia kupigwa kesho Jumanne, huku KMC wakiwa ndio wenyeji wa mechi hiyo ya raundi ya tatu kwa pande zote.

Mwanaspoti ambayo tayari ipo mjini hapa imeshuhudia foleni ya mashabiki na wadau wa soka majira ya saa 1 usiku wakiendelea kuchukua tiketi mapema ili kuepuka usumbufu.

Sauti za baadhi ya mashabiki zilisikika wakisema haijalishi kwamba ni usiku ispokuwa wanachotaka ni kuiona Yanga mapema bila bughuza.

Hata hivyo viingilio katika mechi hiyo imeelezwa kuwa ni Sh 7000 mzunguko na 10,000 jukwaa Kuu kwa wale wenye kadi za N-Card vinginevyo gharama zitaongezeka Sh 1000 kila sehemu.

"Tunataka kadi, tunataka kadi tunataka kadi kuiona timu yetu Yanga, hatoki mtu kesho lazima tuvamie kwa wingi" zilisikika sauti na shangwe za mashabiki