Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lwanga, Akpan wapishana Simba

Lwanga, Akpan wapishana Simba

IMETHIBITISHWA kuwa kiungo mkabaji kutoka Uganda, Taddeo Lwanga ataondoka Msimbazi ili kumpisha Mnigeria, Victor Akpan anayekipiga Coastal Union.

Akpan amesainishwa mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo, huku akisubiri kumaliza kibarua chake akiwa na Coastal katika fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho (ASFC) itakayopigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.

Habari kutoka ndani ya Simba zinasema kuwa mabosi wa klabu hiyo wamekubaliana kuachana na Lwanga kwa kumtoa kwa mkopo kwani mkataba wake umebaki mwaka mmoja na nusu na si rahisi kuuvunja kwani gharama itakuwa kubwa zaidi.

Viongozi hao wa Simba wameanza mchakato wa kumtafutia timu Lwanga ili wamtoe kwa mkopo na wameamua kufanya hivyo kutokana na kutoridhishwa na kiwango chake msimu huu tangu alipotoka kwenye majeraha.

Inaelezwa viongozi wa Simba wamefikia uamuzi huo kwa sababu hawawezi kuwa na wachezaji wawili wanaocheza nafasi moja ya kiungo mkabaji na waliamua kumsajili Akpan kuongeza uimara wa eneo la kiungo wa ukabaji kutokana na Lwanga kushindwa kuwa kwenye ubora wake msimu huu.

“Ishu ya Akpan imeshakamilika, ila hajalipwa chake kwani wanasubiri amalize kuitumikia Coastal katika fainali ya ASFC, kisha klabu yake itoe barua ya kumuachia, atapishana na Lwanga ambaye anatolewa kwa mkopo,” kilisema chanzo chetu makini ndani ya Simba.

Chanzo hicho kinasema mbali na uamuzi wa kutaka kumtoa Lwanga kwa mkopo ili kumpisha Akpan, lakini mabosi wa Simba wamekubaliana pia kuachana na Meddie Kagere, huku Chriss Mugalu akiwagawa mabosi wa timu hiyo kwani wanaotaka abaki na wengine wanataka aachwe.

Kuna wanaosema Mugalu ni mmoja ya mastraika wazuri na wenye uwezo wa kufunga ila majeraha yamemfanya ashindwe kufanya vizuri huku wengine wakieleza si moja ya mchezaji anaweza kucheza michezo mfululizo kutokana na shida hiyo.

Kutokana na hilo kwa Mugalu lolote linaweza kutokea ama asaini mkataba mpya au kuonyeshwa mlango wa kutoka kama ilivyokuwa kwa Pascal Wawa, Rally Bwalya na Benard Morrison.

Mugalu alitafutwa jana na kusema bado hafahamu hatima yake kwa msimu ujao kutokana na mkataba wake wa awali kufikia ukingoni mwishoni mwa msimu huu na amewapa nafasi kubwa Simba kabla ya kufanya uamuzi mwingin wowote.

“Tusubiri kwanza tuone viongozi wangu wa Simba watanieleza jambo gani kuhusu mkataba mpya baada ya hapo ndio nitakueleza kilicho mbele yangu kama nitabaki hapa au nitakwenda kutafuta maisha sehemu nyingine kwani mpira ndio ulivyo,” alisema Mugalu.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez alisema kipindi hicho yupo kwenye wakati mgumu kukamilisha usajili wa wachezaji wapya wanaowahitaji pamoja na kocha atakayekuja kuifundisha timu yao msimu ujao.

“Baada ya kumaliza hilo tutakuwa kwenye utulivu wa kufanya uamuzi wa nyota ambao hatutaendelea nao msimu ujao kutokana na wale wanaomaliza mikataba au vinginevyo,” alisema.