Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Keown: Arsenal wamepigwa, Lille inawacheka tu

Muktasari:

Beki wa zamani wa The Gunners amesema mchezaji ghali zaidi wa klabu hiyo ameshindwa kuthibitisha kama ana thamani hiyo, ila amevutiwa na viwango vya beki mpya wa kushoto Kieran Tierney

London, England. Lille "Wanacheka tu wakiichungulia akaunti yao ya benki ilivyonona” linapokuja suala la uhamisho wa Nicolas Pepe, amesema Martin Keown, huku Arsenal wakiaminika kuwa wamelipa pesa nyingi kuliko thamani halisi ya mchezaji huyo anayecheza chini ya kiwango waliyemnunua kwa Pauni 72 milioni.
Arsenal waliweka rekodi binafsi ya uhamisho walipomsajili winga huyo wa Ivory Coast na kuwa mchezaji ghali zaidi katika historia ya klabu hiyo ya London katika dirisha la uhamisho lililopita.
Pepe, 24, alitua kwa mbwembwe Emirates Stadium, akitajwa kugombewa na klabu nyingi kubwa za Ulaya.
Mambo makubwa yalitarajiwa London Kaskazini, lakini winga huyo kishada amekwama kufikia wakati huu.

Amefunga bao moja tu katika mechi tisa alizocheza, na ni la penalti aliyopewa apige na Pierre-Emerick Aubameyang.
Aliondoka mikono mitupu pia katika mechi ya usiku wa Alhamisi wakati Arsenal wakiifunga kirahisi Standard Liege 4-0 katika mechi yao ya Europa League, jambo lililomuibua gwiji Keown akisema kwamba Pepe ameshindwa kuonyesha kama ana thamani ya pesa iliyomwagwa kumsajili.
“Pepe, ataweza kuingia kikosini? Pesa nyingi imetumika kumsajili na sasa Lille watakuwa wanacheka tu wakiangalia akaunti yao (ilivyonona) kutokana na dili hilo.
“Ni mapema sana bado na pengine atabadili mambo, lakini hakika sijaona ninachotarajia kukiona kutoka kwake.”
Wakati akikosoa mchango wa Pepe, Keown amevutiwa na kiwango cha mgeni mwenzake Pepe, Kieran Tierney, 22.
Beki huyo wa kushoto wa kimataifa wa Scotland ameingia kirahisi kikosini baada ya kutua akitokea Celtic akiwa majeruhi, lakini sasa ametumia mechi mbili tu kuthibitisha anamweka Sead Kolasinac katika presha ya kuwania namba hiyo.
Katika mechi hiyo, Tierney alitoa pasi ya bao kwa Dani Ceballos dakika ya 57 huku mabao mengine yalifungwa na kinda Mbrazili, Gabriel Martinelli dakika ya 13 na 16 na jingine Joe Willock dakika ya 22.