Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Karia: Ishu ya GSM bado ipo mezani

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amekiri shirikisho hilo lipo kwenye mazungumzo na Kampuni ya GSM iliyotangaza kujitoa kwenye udhamini mwenza wa Ligi Kuu Bara kwa lengo la kumbakisha mdhamini huyo.

GSM ilitangaza kujitoa kupitia kwa Ofisa Biashara wake, Allan Chonjo aliyethibitisha wamejiondoa kwenye udhamini mwenza baada ya TFF na Bodi ya Ligi kushindwa kusimamia matakwa yaliyopo kwenye mkataba walioingia na wiki iliyopita Mwanaspoti liliripoti kuwepo kwa mazungumzo baina ya pande hizo mbili, huku baadhi ya vigogo wa shirikisho hilo wakificha, lakini jana Karia amekiri jambo hilo na linasimamiwa na kamati maalumu.

Karia aliiambia Mwanaspoti, mazungumzo yanaendelea, japo yeye hahusiki moja kwa moja na kwamba anasubiria yakamilike kabla ya kupewa taarifa.