Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huku Kisiga, kule Coutinho ni noma

Kocha Marcio Maximo akitoa maelekezo ya mwisho kwa wachezaji wa Yanga. Picha na Mpigapicha Wetu

Muktasari:

Mpaka sasa Kisiga wa Simba na Coutinho wa Yanga ndiyo wamedhihirisha umahiri wao wa kufunga magoli kwa mipira ya faulo. Kisiga alifanya hivyo walipotoka sare na Coastal Union wakati Coutinho alitikisa nyavu kwa mpira wa faulo waliichapa Tanzania Prisons kwa goli 2-1.

INAWEZEKANA ulikuwa hujui. Lakini kwa taarifa yako faulo yoyote itakayotokea kwenye mchezo wa leo kwa upande Yanga mpigaji atakuwa, Mbrazili Andrey Coutinho pamoja na Mnyarwanda Haruna Niyonzima ‘Fabregas’ wakati Simba wapigaji ni Shaaban Kisiga na Emmanuel Okwi raia wa Uganda.

Mpaka sasa Kisiga wa Simba na Coutinho wa Yanga ndiyo wamedhihirisha umahiri wao wa kufunga magoli kwa mipira ya faulo. Kisiga alifanya hivyo walipotoka sare na Coastal Union wakati Coutinho alitikisa nyavu kwa mpira wa faulo waliichapa Tanzania Prisons kwa goli 2-1.

Katika mazoezi ya Yanga, yaliyokuwa yanafanyika Uwanja wa Boko Veterani, Coutinho ameonyesha ustadi wa hali ya juu katika kupiga faulo zinazotokea upande wao wa kulia akitumia mguu wake wa kushoto kwa ufundi mno bila kukosa na hata akikosa usababisha hali ya hatari kwenye goli.

Naye Niyonzima ambaye pia ana rekodi ya kufunga bao kali la faulo kwenye mechi yao na JKT Ruvu waliyoibuka ma ushindi wa magoli 2-1, amekuwa shujaa kwa kuzipiga vyema faulo zinazotokea upande wao wa kushoto.

Mfano, katika mazoezi yao ya juzi (Alhamisi) jioni na jana asubuhi , baada ya kumaliza kucheza mechi ya wenyewe kwa wenyewe, Kocha msaidizi wa Yanga, Mbrazili Leonardo Neiva aliwachukua, Coutinho, Niyonzima na Nizar Khalfan na kuwapa mazoezi ya kupiga faulo nje kidogo ya 18 na golini huku wakimsumbua golini kipa Deogratius Munishi ‘Dida’.

Coutinho mwenye rekodi ya kufunga bao kali la faulo kwenye mechi yao na Prisons ya Mbeya waliposhinda 2-1, alitengewa mipira minne akatakiwa kupiga faulo kutokea upande wao wa kulia ambazo tatu alipata na moja tu ndiyo alikosa.

Niyonzima naye, alipewa mipira mitatu na kupiga faulo zilizotokea upande wao wa kushoto akapata moja na mbili alikosa, wakati Nizar alipiga faulo nne akakosa zote.

Lakini kama itatokea faulo za mbali kama zaidi ya mita 25 Mnyarwanda Mbuyu Twite atahusika kupiga akisaidiwa na Nizar na hii ni kutokana na nguvu waliyonayo zinazowafanya wawe na uwezo wa kupiga mpira wa kasi wakiwa mbali.

Simba nao wapo  kwenye faulo

Simba, ambayo yenyewe ilijificha nchini Afrika Kusini na kufanya maandalizi yao huko, Kisiga ndiye mwenye majukumu ya kupiga faulo ambazo zimekuwa zikizalisha magoli mara kwa mara. Ustadi wake wa kupiga mipira hiyo unamfanya kuwa miongoni mwa wachezaji hatari kwenye kiungo ya Yanga na amekuwa akiwapa wakati mgumu mabeki na magolikipa kutokana na kucheza mpira wa akili na mahesabu.

Lakini washambuliaji wao nao, Okwi pamoja na Ramadhani Singano ‘Messi’ nao watahusika kupiga faulo, wakati zile za mbali zitapigwa na Jonas Mkude.

Kwenye upigaji wa penalti

Kiungo huyo Mbrazil, Coutinho ndiye amekuwa kinara na mpigaji mzuri wa penalti kwani baada ya zoezi hilo la faulo kumalizika juzi, alipiga penalti nne na akapata zote. Niyonzima alipiga penalti tatu, akapata mbili na kukosa moja wakati Nizar alipiga moja ambayo alifanikiwa kufunga.

Upande wa pili ambako kulikuwa na kipa Juma Kaseja, Kocha Mkuu Mbrazil Marcio Maximo aliwakusanya, Said Bahanuzi, Jerry Tegete, Oscar Joshua, Hamis Kiiza (raia wa Uganda) na Mrisho Ngassa ambao nao walifanya zoezi la kupiga penalti tatu kila mmoja. Katika penalti hizo, Bahanuzi, Tegete, Oscar na Msuva kila mmoja wao, walipata mbili na kukosa moja wakati Ngassa alipata moja na kukosa mbili.

Penalti za Simba

Simba nayo ina wachezaji mahiri linapofika suala la penalti. Kama unakumbuka shujaa wa mchezo wa Simba na Yanga uliomalizika kwa Simba kushinda goli 5-0.

Emmanuel Okwi alikuwa mmoja wa wapiga penalti ambao mpaka leo anakumbukwa kwa penalti yake hiyo. Simba walikuwa wakimtumia Okwi kupiga penalti siku za nyuma lakini pia wapigaji wengine wazuri ni Amissi Tambwe na Kisiga.