GSM aibuka kwa Mkapa

WACHEZAJI wa Yanga jana waligawa jezi kwa mashabiki wao waliofika kwenye Uwanja wa Mkapa kushuhudia mechi yao ya Ligi Kuu Bara mzunguko wa nane.

0Kitendo hicho kilifanyika baada ya kikosi cha Yanga pamoja na benchi la ufundi kupiga picha ya pamoja kabla mechi hiyo haijaanza.

0Jezi ambazo wachezaji wa Yanga waligawa ni hizi mpya ambazo zinatumika msimu huu hali iliyowafanya mashabiki kugombea ili kila mmoja apate.

0Utaratibu wa wachezaji wa Yanga kugawa jezi ulianza wakati mchezaji wao Paul Godfrey ‘Boxer’ alipofiwa na baba yake ambapo wachezaji waligawa jezi zenye jina la mchezaji huyo mgongoni.


GSM YAIBUKA

Wiki sasa kumekuwepo na malalamiko kutoka upande wa Simba kuhusu mkataba wa udhamini wa Ligi Kuu Bara ambao Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wamesaini na GSM na katika mchezo huo ilidaiwa kuwekwa mabango ya mdhamini huyo pamoja na jezi kuwekwa nembo ya mdhamini jambo ambalo walilipinga.

Hata kwenye mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya maandalizi ya mechi hiyo, Simba waligomea wakitaka bango la mdhamini mwenza GSM litolewe, hivyo hata mabango yaliyowekwa uwanjani ilibidi yaondolewe kabla ya mechi hiyo na kubaki ya mdhamini mkuu NBC.

Wakati mabango hayo yakiondolewa siku ya mechi, wachezaji wa Yanga wao walivaa jezi ambazo ziliwekwa nembo ya mdhamini mwenza huyo hali ambayo iliamsha shangwe kwa mashabiki wao wakiimba jina la mdhamini huyo.