Gor Mahia yaonywa mapema

Monday January 11 2021
gor pic

MTANZANIA anayeichezea KCB ya Kenya, Islam Rama Abdi ameionya mapema Gor Mahia kwa kusema wasitegemee kuwashusha kwenye kilele cha msimamo wa Ligi hiyo.

KCB wanaonekana kuwa moto wa kuotea mbali kwenye Ligi hiyo baada ya kuibuka na ushindi kwenye michezo sita mfululizo na kujikusanyia pointi 18.

Abdi ambaye ni beki wa kati, alisema malengo yao ni kutwaa ubingwa wa Ligi ya Kenya ambayo imekuwa ikitawaliwa kwa miaka mingi na Gor Mahia.

“Tumekuwa kukipambana kila mchezo kwetu kama fainali, Ligi ni ngumu sana lakini tunamshukuru Mungu kwa kutusaidia na kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wetu uliopita Jumamosi dhidi ya Bidco United,” alisema.

Gor Mahia ipo kwenye hatari ya kushuka daraja ikiwa na pointi tatu kwenye michezo miwili waliyocheza, mabingwa hao watetezi wanaviporo vya michezo minne mkononi kutokana na kushiriki kwao kwenye mashindano ya Kimataifa.

Advertisement