Chege: Wasanii tufanye kazi zinazoishi

Muktasari:
- Kama kuna kitu anakiamini mwanamuziki Chege Chigunda ni kufanya vitu vyenye tija vitakavyoendelea kulinda heshima mbele ya jamii inayowazunguka.
KAMA kuna kitu anakiamini mwanamuziki Chege Chigunda ni kufanya kazi kwa bidii ambazo zitakuwa zinaleta mapinduzi kwenye jamii na sio kelele nyingi zitakazosahaurika muda mfupi.
Ushauri wake kwa mastaa ambao ni kioo cha jamii, Chege aliwataka wafanye vitu vya kuleta maendeleo nchini akitoa sababu kwamba ni rahisi kueleweka kutokana na kazi zao.
"Tuna nguvu kubwa ya kufanya jamii yetu ikawa na nguvu ya jambo fulani kupitia sanaa zetu, ndio maana unakuta muziki ya watu wa zamani inapendwa sana ndani yake kuna ujumbe,"
"Ujumbe wenye tija una nguvu ya kuishi mioyoni mwa watu kuliko kelele ambazo siku mbili zinasahaurika, ili tuendelee kupata heshima lazima vitu vyetu viwe na thamani kubwa,"
"Muziki una nguvu kubwa, unabadilisha mioyo ya watu, unaleta mtazamo mpya kwenye jamii, unaleta faraja na furaha, hivyo lazima tutumie vyema ili kuwa msaada kwa wale wanaounga mkono kazi zetu,"alisema.