Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chama: Simba hii ni moto

Chama: Simba hii ni moto

KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama amekiangalia kikosi cha timu hiyo na kusema msimu ujao heshima itarejea Msimbazi.

Chama aliyeuzwa mwanzoni mwa msimu uliopita kwenda RS Berkane ya Morocco na kurejea katika dirisha dogo, aliishuhudia timu hiyo ikipoteza mataji matatu iliyokuwa inayashikilia kwa Yanga ikiwamo Ngao ya Jamii, Ligi Kuu Bara na Kombe la ASFC.

Akizungumza na Mwanaspoti kutoka kambini Misri, Chama alisema ujio wa wachezaji wapya na hata kocha umeongeza ari kwa wachezaji kwanye maandalizi yao.

Kiungo huyo Mzambia alisema: “Tupo vizuri kwa mapambano. Binafsi najiona kuwa fiti na tayari kwa msimu ujao.

“Kiukweli nimefurahia usajili uliofanywa na ninaamini timu itakuwa na matokeo mazuri msimu ujao, kikubwa mashabiki ni kuendelea kutuunga mkono.”

Chama alisema kwa aina ya wachezaji walipo sasa na kile wanachokipata kwa kocha Zoran Maki, anaamini watarejesha heshima ya klabu hiyo baada ya kuyumba msimu uliopita.