Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam inatema nyota wa kigeni

AZAM FC imeanza hesabu za kuboresha kikosi chao na katika ramani ya usajili wao kuna mastaa watatu kutoka mataifa mbalimbali watapisha nafasi.

Taarifa kutoka kikosi kazi cha maskauti wa timu hiyo wanaosimamia usajili, mastraika wawili wamewekwa katika listi ya kuondolewa ambao ni Obrey Chirwa na Mpiana Mozinzi.

Hata hivyo, kurejea kwa kasi ya Mozinzi ambaye wiki iliyopita alipiga bao mbili dhidi ya Gwambina imeonekana kuwashtua mabosi wa timu hiyo na kuanza kufikiria mara mbili juu ya uamuzi wao huo.

Mkataba wa Mozinzi na Azam unafikia tamati Desemba mwaka huu na Azam inafikiria kama atashindwa kuamka zaidi kuna uwezekano akapisha nafasi.

“Unajua wako ambao wanataka Mozinzi apewe muda pia wapo wanaotaka aachwe na kuanza kufunga juzi mabao mawili kumeleta mvutano wa hatma ya Mozinzi,” alisema bosi huyo.

Mbali na washambuliaji hao pia beki Yakubu Mohammed yumo katika kundi la wanaoachwa mwisho wa msimu baada ya sasa kushindwa kupenya kikosi cha kocha George Lwandamina.

Tayari Mtendaji Mkuu wa Azam Abdukarim Amin ‘Popat’ alikuwa nchini Zambia akifuata viungo wawili na anatarajiwa kurejea nchini leo.

Popat nchini Zambia aliwafuata viungo Collins Shikombe na Benson Sakala ambao pia ni wachezaji wa timu ya taifa ya Zambia ‘Chipolopolo.