Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aucho, Djuma washtua Yanga

Aucho, Djuma washtua Yanga

VIKOSI vya Yanga na Geita Gold tayari vipo jijini Mwanza kwa ajili ya mechi yao itakayopigwa leo, huku mastaa wawili wa Jangwani, Khalid Aucho na Djuma Shaban wakishtua mashabiki wa timu hiyo baada ya kukosekana kwenye msafara.

Yanga iliondoka jijini Dar es Salaam na kutua jijini Mwanza asubuhi na kupokewa na mashabiki lukuki wa klabu hiyo, lakini Aucho na Djuma hawakuwepo katika msafara huo ikielezwa wana matatizo binafsi.

Aucho na Djuma waliachwa kwenye msafara wa wachezaji 22 waliondoka Dar na kutua Mwanza jana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Air Tanzania na kwa mujibu wa Meneja wa Yanga, Saleh Hafidh alifichua Aucho anaumwa.

“Hayupo sawa kiafya ndio sababu ya kumwacha,” alisema Hafidh akitolea ufafanuzu juu ya fundi huyo wa mpira kutoka Uganda mwenye mabao matatu Bara, lakini kwa upande wa Djuma, meneja huyo hakusema lolote akiwaomba radhi waandishi kwani alikuwa akiwahi ndani ya ndege.

Ikiondoka jijini Dar es Salaam saa 2 asubuhi msafara wao viongozi waliokuwapo ni Injinia Hersi Said na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Senzo Mazingisa na mchezaji wa kwanza kuwasili uwanjani hapo alikuwa Fiston Mayele aliyeuzungumzia mchezo huo wa kesho akisema;

“Utakuwa mgumu, licha ya wengi kutupa nafasi kubwa kushinda, Geita ni timu ngumu na inafanya vizuri, tumejiandaa kukabiliana nao ili kuendelea kuweka hai matumaini yetu kwenye ubingwa.”

Senzo kwa upande wake alisema; ”Mchezo utakuwa mgumu lakini tumefanya maandalizi ya kuhakikisha tunafanikiwa kupata pointi tatu.”

Wachezaji walioondoka na kutua Mwanza saa 4 asubuhi na kupokewa kwa mbwembwe ni pamoja na Diarra Djigui, Abuutwalib Mshery, Kibwana Shomari, Paul Godfrey, Yassin Mustapha, David Bryson na Bakari Mwamnyeto.

Wengine, Yannick Bangala, Ibrahim Abdallah ‘Bacca’, Dickson Job, Saido Ntibazonkiza, Feisal Salum, Denis Nkane, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Chico Ushindi, Mapinduzi Balama, Dickson Ambundo, Heritier Makambo, Deus Kaseke, Farid Mussa, Eric Johola na Zawadi Mauya.


MWANZA SHANGWE

Mara Yanga ilipotua jijini Mwanza ilipelekwa Hoteli ya Antelope kwa ajili ya kupumzika, huku mashabiki wakiisindikiza na misafara ya magari na bodaboda huku shangwe likinogeshwa zaidi na wimbo wa ‘Yanga Tamu’ ulioimbwa na Marioo.

Kocha Fred Felix ‘Minziro’ ameonekana kupania kulipa kisasi cha kufungwa bao 1-0 katika mchezo wao wa kwanza.