SIMBA ilipoteza mechi ya kwanza kwenye mechi za makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kunyukwa na RS Berkane kwa mabao 2-0, lakini ikajifariji kwa kusema itamaliza kazi Kwa Mkapa.
Simba ilikumbana na kipigo kwenye Uwanja wa Berkane, Morocco katika mechi ya Kundi D iliyopigwa kuanzia saa 4:00 usiku na kuifanya ing’oke kileleni hadi nafasi ya pili ikisaliwa na pointi 4 sawa na ilizonazo USGN ya Niger iliyoitoa nishai ASEC Mimosas ya Ivory Coast kwa kuilaza 2-0 katika mechi ingine ya kundi hilo.