Simba Queens ina kibarua kizito mbele yao kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika imebakiza mchezo mmoja dhidi ya Green Buffaloes ya Zambia ambao utakua wa kukata na shoka.
Simba ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi A na pointi tatu sawa na Green Buffaloes iliyo ya pili ikiwa na utofauti wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Mchezo wa mwisho utazikutanisha timu hizo ambazo zinatafuta nafasi ya kusonga mbele ikiwa ASFAR ndio anaongoza kundi kwa pointi sita baada ya kucheza mechi mbili.