Bosi wa lebo ya Konde Music Worlwide, Rajab Abdul ’Harmonize’ amethibitisha kuachana na msanii wake mwingine Angelina Samson ’Anjella’.
“Nilikutana na Anjella akiwa amejikatia tamaa akiwa na ndoto kichwani, sikujiangalia nina kiasi gani, niliamini kwakuwa watu wapo wananisapoti bila kuwalipa senti tano basi watasapoti kipaji cha dada Anjella.
“Nilichoangalia ni ndoto hasa za mtoto wa kike, nimejitahidi kufanya ya uwezo wangu najua kuna wenye uwezo mkubwa kunizidi.
“Ukizingatia nimeanza juzi kama kuna anayeweza kumuendelezea kipaji chake ni faraja kwangu asisite kujitokeza, puuzia siasa zakusema sijui namdai, hela sijawahi kumdai hata senti, ”ameandika Harmonize.