Timu ya taifa Croatia imetinga nusu Fainali ya Kombe la Dunia 2022 baada ya kuitupa Brazil nje kufuatia ushindi wa penalti 4-2, mchezo uliochezwa Uwanja wa Education City.
Mchezo huo ulimalizika kwa dakika 90 kwa suluhu na kulazimika kucheza zingine 30 na kutoa sare ya bao 1-1.
Brazil imetolewa kwenye hatua ya penalti baada ya Rodrygo na Marquinhos kupoteza mikwaju ya penalti.